Msemaji mkuu wa serikali Dokta Hassani Abbas amesema
utaratibu unawekwa ili kuwatambua Rasmi waandishi wa habari za mitandao ya kijamii (Bloggers) wanaohusika
kuandika taarifa mbalimbali za kuhabarisha.
Dokta Abas ameyasema hayo wakati alipotembelea kituo cha
Radio Triple A iliyopo Arusha ambapo mmoja wa mtangazaji wa radio hiyo Alphonce
Saul ambaye ni mmliki wa Blog iitwayo Kusaganews ambaye alitaka kujua ni vipi
watu hao watatambuliwa rasmi na serikali kama vyombo vingine vya kuhabarisha
jamii.
Akijibu swali la Mtangazaji huyo Dokta Amesema kuwa kwasasa
wametengeneza kanuni ambazo ziko kwa mwanasheria ambazo zinaitwa (Online Content
Regulation)ambazo zinahusu namna ya kuwatambua wandishi wa habari (NEWS)wa
mitandaoni ambao pia watapewa vitambulisho maalum (Press card) ili watambuliwe
rasmi.
Ameongeza kuwa kanuni hizo zitahusu wamiliki wa Blogs
pamoja , Radio za mitandaoni (online Radio)pamoja na Televisheni za mitandano
Tv Online)ambapo utaratibu huo unaendelea.
Dokta Hassani Abasi amefanya ziara katika radio Sunrise
Arusha na Triple A Radio Arusha ambapo pia amepata vipndi vya kuzungumza hewani
moja kwa moja na wananchi.
WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAONI (BLOGGERS) WAANZA KUTAMBULIKA NA SERIKALI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment