Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao wamepanga njama za
kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya
Mwigulu ametoa hiyo wakati alipokuwa
akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli aliyopo Mkoani Singida katika ziara
yake ya kikazi ambapo leo hii (Machi 11, 2018) amezindua kiwanda cha Alizeti
Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika maandamano hayo ni namna ya watu
wanatakanywa tawanywa ili kusudi waje kulalamika kuwa serikali ndio imeuwa watu
wake.
"Njama hiyo tumeiona na mimi
nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama ya kuua ni kosa, wachukue
hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi
yetu ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma. Watu wanataka mikusanyiko ili
wafyatue na kuuwa watu ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano
wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa", amesema Mwigulu.
Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea
kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago vinyago vingi
hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na
akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa
ametekwa. Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?, watu wanatafuta njia za kuchafua
taswira ya nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo,
si jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano wala
hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana".
Aidha, Waziri Mwigulu amesema endapo
ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba zao bado sheria itachukua
mkondo wake dhidi ya watu hao.
"Ikitokea hata watu
wakaandamana ndani ya nyumba wakazunguka kitanda na akatokea mtu akaumia, yule
aliyeitisha waandamane pale atakuwa nala kuajibika kwasababu watu wanafanya
mzaha na maisha na dira ya nchi yetu ambapo Rais umejitoa muhanga kwa ajili ya
kutengeneza urithi wa watoto wa Tanzania", amesisitiza Mwigulu.
Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu
amesema yeyote atakayethubutu kutaka kuharibu taifa la Tanzania kwa kufanya
vitendo vya uovu hawatoweza kumuacha salama.
Ukifanya maandamano hata kitandani, utakipata
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment