Baraza la Uuguzi na
Ukunga Tanzania linalaani na linatoa pole kwa Wauguzi kutokana na matukio
yaliyofanywa na viongozi ikiwemo kuwekwa rumande na kupigwa katika mazingira yao
ya kazi.
Taarifa kutoka katika baraza hilo,
iliyotolewa na Lena M. Mfalila imesema kwamba vitendo hivyo ni udhalilishaji na
ni kinyume cha miongozo ya kisheria inayosimamia ushughulikiaji wa tuhuma za
uvunjifu wa nidhamu na sheria wakati wa kazi.
Taarifa hyo imeongeza kwamba kumpiga
mtumishi wakati akiwa kazini ni udhalilishaji na ni kinyume cha sheria.
"Nidhamu ya Wauguzi na Wakunga inasimamiwa na sheria inayoitwa the Nursing
and Midwifery Act, 2010 inayotoa mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu kwa
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania".
Matukio hayo ya udhalilishaji
yanajumuisha tukio lililotokea tarehe 7/3/2018 katika Hospitali ya Wilaya ya
Tandahimba ambapo Muuguzi Amina Luena Nicodemus aliwekwa ndani kwa amri ya Mkuu
wa Wilaya kwa tuhuma za kuuza nguo za watoto akiwa kazini. pamoja na lingine
lililotokea tarehe 8/3/2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo
Muuguzi Hilda Ebunka alipigwa na Diwani akiwa kazini akitoa huduma.
Viongozi wa kitaifa, ikiwa ni pamoja
na Mheshimiwa 2 Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -
TAMISEMI na Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa nyakati mbalimbali wamekemea na kusisitiza mamlaka mbalimbali
kuepuka kufanya vitendo vya udhalilishaji wa Wauguzi na Wakunga.
Wauguzi wapewa Pole
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment