Trump atangaza Mpango wa kupambana na wauzaji wa Madawa ya Kulevya

Rais wa Marekani Donald Trump ameeleza mpango wake wa kupambana na wauzaji wa dawa za kulevya chini humo na kudai Bunge lake limetenga jumla ya dola Bilioni 6 za kimarekani kwa lengo la kutatua tatizo hilo.

Trump ametoa kauli hiyo wakati akihutubia huko Manchester na kusema kuwa dawa za kulevya zinagharimu maisha ya watu wengi kutokana na matumizi ya dawa na wanaosababisha vifo hivyo hupewa adhabu ya muda mfupi.

Aidha Trump amefafanua kwamba tayari Bunge lake limetenga kiasi cha dola za Marekani bilioni sita kwa ajili ya kupambana na tatizo hilo ambapo ametaka kuwepo na umakini katika utolewaji wa adhabu kali sambamba na ile ya kifo kwa wauzaji wa dawa za kulevya.


Katika kampeni zake za urais Donald Trump alitoa ahadi nzito zikiwemo kujenga ukuta ili kudhibiti wahamiaji haramu, kutengua mpango wa afya wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Obama Barrack na ile ya  Marekani kwanza.
Trump atangaza Mpango wa kupambana na wauzaji wa Madawa ya Kulevya Trump atangaza Mpango wa kupambana na wauzaji wa Madawa ya Kulevya Reviewed by KUSAGANEWS on March 20, 2018 Rating: 5

No comments: