Serikali yapiga Marufuku shule kupokea wanafunzi wasiopimwa Kifua Kikuu

Serikali imepiga marufuku wamiliki wa shule kupokea wanafunzi ambao hawana vibali vyakudhibitisha kuwa wamepima ugonjwa wa kifua kikuu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kwenye uzinduzi wa dawa za ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto ambapo amesema uwamuzi huo umekuja baada yakuona ripoti ya shirika la afya duniani WHO zinaonyesha jumla ya wagonjwa milioni 1.3 wamefariki kwa ugonjwa huo kwa mwaka wakati Tanzania inakadiriwa vifo 28 elfu hutokea kwa mwaka kutokana na ugonjwa huo na asilimia 10 ya wagonjwa ni watoto.

Amesema ugonjwa huo ndio unaongoza kwa kuuwa watu wengi dunia hali ambayo kama tahadhari za haraka hazijachukuliwa ni wazi idadi kubwa ya watu watapoteza maisha.


Kwa upande wake mganga mkuu wa serikali Dkt. Muhamed Bakari Kambi amewataka wanaotumia dozi kuhakikisha wanazimaliza ili kumaliza ugonjwa mwilini.
Serikali yapiga Marufuku shule kupokea wanafunzi wasiopimwa Kifua Kikuu Serikali yapiga Marufuku shule kupokea wanafunzi wasiopimwa Kifua Kikuu Reviewed by KUSAGANEWS on March 20, 2018 Rating: 5

No comments: