Watu 2 majambazi wauwawa na Polisi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema watu wawili wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi wameuawa wakati wakijibizana kwa risasi na Polisi wakati walipokuwa wanakwenda kuwaonesha silaha walizokuwa wamezificha katika pori Kasulu

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Maltin Otieno leo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kusema ilipofika majira ya saa 5:00 usiku jana (Machi 19, 2018) kwenye pori la Makere katika Kijiji cha makere wilayani Kasulu watu wawili ambao ni Norbert Andrew na Bukuru Stiven ambaye ni mkimbizi kambi ya Nyarugu waliuawa kwa kushambuliwa na majambazi wenzao wakati wakienda kuwaonesha Polisi silaha ambazo walikuwa wamezificha porini.
Aidha, Kamanda Otieno amesema watu hao walikamatwa katika tukio moja la kuvunja kibanda na kuiba na
mmoja wa majambazi hao waliangusha simu eneo la tukio iliyowezesha polisi kumkamata na baada ya kuhojiwa na Polisi walikiri kuhusika na matukio mauaji, na uvamizi katika nyumba za watu wilayani hapo.

"Baada ya mahojiano hayo mtuhumiwa aliwaongoza Polisi mpaka kambi ya Nyarugusu na kufanikisha kukamatwa mtuhumiwa mwingine na ilipomalizika zoezi la kupekuliwa walikutwa na silaha walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu na kueleza kuwa kuna eneo jingine silaha tano zimefichwa ambapo ni porini, polisi waliondoka na watuhumiwa hao na walipofika maeneo ambayo wameficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao", ame
Watu 2 majambazi wauwawa na Polisi Watu 2 majambazi wauwawa na Polisi Reviewed by KUSAGANEWS on March 20, 2018 Rating: 5

No comments: