Tetemeko la ardhi latikisa Kagera,Mwanza


Tetemeko la ardhi lililodumu kwa takribani dakika moja usiku wa kuamkia leo Machi 25, 2018 limetokea Mkoa wa Mwanza, Kagera na Geita, kuzua taharuki kwa wakazi wa mikoa hiyo, huku baadhi  wakijaribu kukimbia nyumba zao kwa nia ya kujiokoa

Hata hivyo hakuna madhara ya vifo au uharibifu ulioripotiwa hadi jana

Jiolojia Mwanandamizi kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Gabriel Mbogomi amesema tetemeko hilo lina ukubwa wa richa 4.6 na lilikuwa likitokea Kaskazini Magharibi ya Mji wa Kahama kuelekea kusikojulikana

Kwa mujibu wa GST, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotokewa na tetemeko la ardhi kutokana na kuwa sehemu ya mkondo wa Bonde la Ufa.

Tetemeko la ardhi latikisa Kagera,Mwanza Tetemeko la ardhi latikisa Kagera,Mwanza Reviewed by KUSAGANEWS on March 25, 2018 Rating: 5

No comments: