Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi Mkuranga kufuatia ajali iliyouwa watu 26

Rais John Magufuli leo Jumapili Machi 25 amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaristi Ndikilo kufuati ajali iliyotokea na kusababishsa vifo vya watu 26.

Ajali hiyo iliyotokea  saa tatu usiku ilihusisha gari aina ya Hiace iliyokuwa imebeba abiria kugongana na lori lililokuwa limebeba chumvi katika Kijiji cha Mparange Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani
“Nimesikitishwa sana na taarifa ya vifo vya watu 26 waliopoteza maisha kwenye ajali ya barabarani iliyotokea huko Mkuranga mkoani Pwani, tumepoteza idadi kubwa ya Watanzania wenzetu na nguvu kazi ya Taifa,” amesema Rais Magufuli

Rais katika salamu za rambirambi alizotoa amemtaka Mhandisi Ndikilo kumfikishia salamu za pole kwa familia za marehemu ndugu jamaa na marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo pamoja na kuvitaka vyombo vya usalama kushughulikia usalama wa barabarani na kuchunguza ajali hiyo pamoja na kuchuku hatua stahiki
“Naungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao na watu aliowategemea,”amesema Rais Magufuli

Amewaombea marehemu wote wapumzike mahali pema peponi na majeruhi tisa wa ajali hiyo wapone haraka ili waungane na familia na jamaa zao katika shughuli zao za kila siku
Basi hilo lilikuwa likitokea Mkuranga kuelekea Kimanzichana wakati lori lilikuwa likitoka Lindi kuelekea Dar es Salaam.
Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi Mkuranga kufuatia ajali iliyouwa watu 26 Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi Mkuranga kufuatia ajali iliyouwa watu 26 Reviewed by KUSAGANEWS on March 25, 2018 Rating: 5

No comments: