Shirikisho la soka
nchini Tanzania TFF leo limetangaza kuwa timu ya Taifa ya Vijana wenye umri
chini ya miaka 13 (U13) inatarajiwa kushiriki michuano ya vijana inayoandaliwa
nchini Ubeligji.
TFF imeeleza kuwa michuano hiyo
itashirikisha timu za vijana za nchi zaidi ya 10 kutoka mataifa mbalimbali na
itafanyika mwezi Agosti, 2018 nchini Ubeligji.
Michuano hiyo inatarajia kukusanya
timu za vijana kutoka taifa moja la bara la America ya Kusini, Asia pamoja na
zingine za Ulaya huku Africa ikiwa Tanzania pekee ndio imepata mwaliko huo.
Taarifa ya TFF imeeleza kuwa
michuano hiyo ni maalum kwa kuwajenga wachezaji hao kwaajili ya soka la
kulipwa, ambapo wanapata fursa ya kukutana na mawakala wa wachezaji na timu
mbalimbali hivyo inaweza ikafungua milango kwa vijana wa Tanzania.
Timu mbalimbali za taifa za vijana
kuanzia miaka 13, 16 na 20 zipo kambini kwaajili ya michuano tofauti tofauti
ambapo Serengeti Boys inajiandaa na michuano ya CECAFA kwa vijana
itakayofanyika Burundi.
Tanzania kucheza na timu za Ulaya na Amerika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment