Mwenyekiti wa kamati ya
kudhibiti maendo ya ngono Dr. Annette Kezaabu, ameishauri serikali nchini
Uganda kupitia wizara ya Elimu na michezo, kuingiza somo la filamu za ngono
(pornography) kwenye mtaala wa shule za msingi na sekondari, kwani itasaidia
kufundisha watoto madhara yake na
kujua namna ya kujiepusha.
Akizungumza kwenye mkutano na
waandishi wa habari katika hoteli moja huko mjini Mbarara nchini Uganda, Dr.
Kezaabu amesema watu wengi wameathirika kwa filamu za ngono kupitia njia mbali
mbali wanazoweza kuzipata, ingawa walishaahidi kulimaliza kutokana na sheria
zilizopo.
Pia Dkt. Kezaabu amesema kwamba
Mkurugenzi wa maadili na masuala ya dini wa Ofisi ya Rais, mchungaji Canon
Aaron sasa anahamasisha umma kuhusu sheria ya kupinga filamu za ngono, na
kuonya kwamba yeyote atakayekiuka atakamatwa na kushtakiwa.
Uganda Wataka somo la ngono kuwekwa kwenye mtaala
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment