Mwanza. Watu 20
wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema akiwemo diwani wa Kata ya Mabatini, Deo
Mbibo wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa walipokuwa wameenda kuhani
msiba wa mwanachama mwenzao.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti
wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Leonard Nundi amesema tukio hilo limetokea leo
Machi 13, saa kumi jioni ambapo wafuasi hao wakiwa zaidi ya 500 walienda
kuhani msiba huo na ghafla polisi waliwavamia na kumtaka mfiwa kuongea naye
“Chanzo cha vurugu ni baada ya
askari hao kuvamia msibani na kumhitaji mfiwa ambaye ni Laurent Chiro kwa
ajili ya mazungumzo, waliposhindwa kuelewana walimchukua diwani na viongozi
wengine waliokuwa meza kuu na kuwapandisha kwenye gari la polisi,” amesema
Nundi.
Amesema wanachama waliokuwa
msibani waliogomea kitendo hicho na kuanza kuwarushia mawe polisi ambao nao
walianza kujihami kwa kupiga mabomu ili kuwatawanya.
Akizungumzia tukio hilo, kamanda
wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi pamoja na kudai yuko wilayani Kwimba,
lakini amesema wafuasi hao wamekuwa na kawaida kukusanyika na kufanya vikao
vyao vya kisiri
Mmoja wa wanachama aliyekuwa eneo
la tukio, Emmanuel Tumbo amesema wafuasi hao wametoka katika kata zote 18 za
Jiji la Mwanza ambao wamejiwekea utaratibu wa kuhani misiba inapotokea kwa
mwanachama anayefiwa au kufariki dunia
|
WAFUASI NA VIONGOZI 20 WA CHADEMA MIKONOI MWA POLISI MWANZA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment