Serikali imepanga kukusanya na kutumia
Sh32.476 trilioni mwaka ujao wa fedha wa 2018/19
|
Akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na kiwango cha ukomo wa bajeti kwa mwaka 2018/19, waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema ukomo wa bajeti umezingatia upatikanaji wa mapato.
Dk Mpango amesema katika mwaka huo Serikali
imepanga kutumia Sh20.468 trilioni kwenye matumizi ya kawaida sawa na asilimia
63 ya bajeti yote.
Matumizi hayo amesema yanajumuisha Sh10
trilioni zitakazolipa deni la Taifa na Sh7.369 trilioni mishahara ya watumishi
wakati Sh3.094 trilioni zikielekezwa kwenye matumizi mengine.
Dk Mpango amesema Serikali itatumia Sh12
trilioni sawa na asilimia 37 kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kiasi hicho, amesema kinajumuisha Sh9.876
trilioni sawa na asilimia 82.3 kutoka vyanzo vya ndani na Sh2.13 trilioni sawa
na asilimia 17.7 kutoka nje.
Jumla ya mapato ya ndani pamoja na makusanyo
ya halmashauri yanatarajiwa kuwa Sh20.894 trilioni ambayo ni sawa asilimia 64
ya bajeti yote
“Kati ya mapato hayo yatokanayo na kodi
yanatarajiwa kuwa Sh18 trilioni sawa na asilimia 13.6 ya Pato la Taifa,”
amesema.
Amesema mapato yasiyo ya kodi yanatarajiwa
kufika Sh2.158 trilioni wakati vyanzo vya halmashauri vikikusanya Sh735.6
bilioni.
Mpango amesema vyanzo vingine
vinavyotarajiwa kufanikisha utekelezaji wa bajeti hiyo ni misaada na mikopo
yenye masharti nafuu kiasi cha Sh2.676 trilioni kutoka kwa washirika wa
maendeleo ambazo ni sawa na asilimia nane ya bajeti hiyo.
Katika mwaka ujao, amesema Serikali
inatarajia kukopa Sh5.793 trilioni kutoka soko la ndani ambazo kati ya hizo,
Sh4.6 trilioni zitatumika kulipia hati fungani na dhamana za Serikali zinazoiva.
Sh1.193 trilioni zinazozidi kwenye mikopo
hiyo ya ndani ambazo ni sawa na asilimia 0.9 ya Pato la Taifa, amesema ndilo
deni jipya
“Ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa
miundombinu, Serikali inatarajia kukopa Sh3.111 trilioni kutoka soko la nje,” amesema
Serikali kukusanya Shilingi Trilioni 32 kwa mwaka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment