Waziri wa Fedha na Mipango, Dk
Philip Mpango amesema hadi Desemba 2017, deni la Taifa lilikuwa limefikia
Sh47.756 trilioni na tathmini zinaonyesha bado ni himilivu.
Akiwasilisha mapendekezo ya
Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ukomo wa bajeti ya Serikali kwa
mwaka 2018/19 mjini hapa leo Machi 13, 2018, Dk Mpango amesema deni la nje
lilikuwa Sh34.148 trilioni sawa na asilimia 71.5 na deni la ndani ni
Sh13.607 trilioni sawa na asilimia 28.5.
Hata hivyo amesema uwiano wa deni
hilo na Pato la Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/18 ni asilimia 34.4
ikilinganishwa na ukomo ambao ni asilimia 56
“Uwiano wa deni la nje na mauzo ya
nje ni asilimia 81.1 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 150. Hii inamaanisha
kuwa uwezo wetu wa kulipa deni bado ni imara,” amesema.
Amesema Serikali inaendelea
kuchukua tahadhari kwa kukopa kwenye vyanzo vyenye masharti nafuu kuhakikisha
mikopo hiyo inaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
|
|
Dokta Mpango Deni la Taifa ni himilivu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment