Polisi katika wilaya ya Mpigi wamemkamata mzee moja mwenye umri wa miaka 69 anaanyejulikana kwa jina la Vicent Ssenonga, ambaye ni mganga wa kienyeji kwa kumpa ujauzito binti yake wa kumzaa mwenyewe.
Kwa
mujibu wa polisi wa kituo cha Buwama ambako mzee huyo anazuiliwa, wamesema
walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa mzee huyo anamnyanyasa binti
yake huyo ambaye amemgeuza mke wake, aliyeanza kufanya naye ngono tangu akiwa
na miaka 13 mpaka sasa ana miaka 20, huku wakiwa wamezaa watoto watatu.
“Kumuoa na kumtesa
mtoto wake mwenyewe, kiasi kwamba hampi chakula na huduma za afya, hatukuweza
kuvumilia na kwenda kumchukua huyu mzee. Tumeambiwa kuwa amemtumia huyu binti
kwa miaka 7 sasa tangu akiwa na miaka 13, na tunachunguza taarifa kuwa
amemuambukiza HIV”, amesema Bwana Jospeh Kakama ambaye ni polis wa zamu wa
kituoni hapo.
Naye mwenyekiti wa
kijiji Bwana Robert Ssemuju amesema mganga huyo alikuwa akiishi na binti yake
huyo pekee, baada ya kuwapa talaka wake zake sita, na watoto wake kutawanyika
kutafuta maisha huko Kampala na sehemu zingine.
“Ssenonga amekuwa
akimtishia huyu binti asiseme chochote kwa watu, lakini kutokana na afya yake
ambayo inadhoofu kila siku, ameamua kutuambia na kuamua kuweza kumsaidia yeye
na hawa watoto watatu”, amesema mzee huyo ambaye ni mwenyekiti wa kijiji.
No comments:
Post a Comment