Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa leo Machi 13, 2018 amefunguka na kusema kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi kuhusu taarifa za kutekwa kwa Abdul Nondo umetoa na kuwa mwanafunzi huyo alijiteka mwenyewe.
Mambosasa amesema
hayo wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa Abdul Nondo
alikamatwa huko Mafinga Iringa akiendelea na shughuli zake na kusema hakuripoti
sehemu yoyote kuhusu kutekwa kwake na kudai kuwa wamebaini kijana huyo
alikwenda kwa mpenzi wake ambaye alikuwa akiwasiliana naye mara kwa mara.
"Pengine
alitaka kuzua hilo ili kujipatia umaarufu ila upelelezi uliendelea kubaini kuwa
mwanafunzi huyo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake ambaye alikuwa akiwasiliana naye
mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa hii ni baada ya kufanya uchunguzi wa
kisayansi na kubaini muda ule aliosema ametekwa simu yake imeendelea kuonyesha
mawasiliano aliyokuwa anafanya na huyo binti ambaye alikuwa
amemfuata"
Mambosasa amesema
kuwa walipomkamata walikuwa na mashaka kuwa huenda akawa amepatwa na ugonjwa wa
malaria ya kichwa iliyopelekea kufanya hayo na kudai kuwa alipelekwa hospitali
na kupimwa na kuonekana kuwa mzima asiye na matatizo yoyote ya kiakili.
"Alikuwa ni
mzima wa afya njema na haya aliyafanya kwa makusudi kwa sababu anazozijua yeye
mwenyewe, jeshi la polisi limebaini kuwa mwanafunzi huyo alikuwa huru baada ya
kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, alisafiri akiwa huru na akafika Iringa
akiwa salama, kwa hiyo ni uzushi mtupu uliokuwa na malengo ya hovyo lakini kuna
watu wengine walilishabikia jambo hili wengine huwezi kuamini kwa nafasi zao
walilishabikia jambo hili la hovyo mtu kujizushia jambo"alisema Mambosasa
Nondo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake hakutekwa - Mambosasa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment