Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka 81 jela mfanyabiashara Timotheo
Wandiba baada ya kutiwa hatiani katika mashtaka 27 ya kujipatia Sh2.1 bilioni
kwa njia ya udanganyifu
Mbali ya Wandiba, mahakama hiyo
imewaachia huru washtakiwa wenzake wawili; Dickson Okololo na Simon Efrem
ambao upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo
kuacha shaka.
Akisoma hukumu hiyo leo Machi 13,
2018 iliyoandikwa na Hakimu Joyce Minde, Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri
amesema washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa 82 ambapo upande wa
mashtaka uliita mashahidi 14.
Katika makosa hayo 82, mashtaka 27
ni ya kughushi, 27 ya kutoa hati za uongo, 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu na moja la utakatishaji fedha.
Hakimu Mashauri amesema mahakama
hiyo imemtia hatiani Wandiba katika makosa 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa
upande wa mashtaka.
Katika makosa hayo, Mashauri
amesema katika kila kosa Wandiba atatumikia kifungo cha miaka 3 jela
ambapo jumla itakuwa ni miaka 81, lakini kwa kuwa vifungo hivyo vitakwenda
sambamba atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Pia, hakimu amesema mahakama hiyo
imemuachia huru Wandiba na wenzake, Okololo na Efrem katika makosa mengine
yote baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuyathibitisha pasipo kuacha
shaka.
Katika kesi hiyo washtakiwa
walikuwa wakikabiliwa na makosa 82 ikiwemo kughushi, utakatishaji fedha na
uwasilishaji wa nyaraka za uongo.
Wakati kesi hiyo ikiendeshwa
washtakiwa walikuwa rumande kutokana na kukabiliwa na shtaka la kutakatisha
fedha ambapo kwa mujibu wa sheria halina dhamana
|
AFUNGWA JELA MIAKA 81 BAADA YA KUTIWA HATIANI NA MASHTAKA 27.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment