Mkuu wa Mkoa wa Njombe
Christopher Ole - Sendeka amewaruhusu madereva wa bajaji Mkoani Njombe ambao
walisimamishwa kufanya shughuli zao katika barabara kuu ya Njombe - Songea na
kuruhusu bajaji kuongezwa mpaka bajaji 100 kutoka 55 ambazo zilikuwepo.
Sendeka ameruhusu kufanya kazi
bajaji baada ya kusimamishwa na mamlaka ya usafirishaji wa Majini na Nchi kavu
Sumatra ambapo walisimamishwa kwa mujibu wa sheria ya bajaji na pikipiki ya
mwaka 2010.
Aidha Madereva hao wa bajaji
wamedai kuwa walipeleka katika vituo ambavyo wanadai kuwa havikuwa na
maslahi kwao na kwa biashara yao na hakukuwa rafiki kimiundombinu.
Hata hivyo wamiliki wa bajaji Mjini
Njombe wamesema kuwa kwa muda wa wiki moja hawajaingiza fedha yoyote na kusema
serikali imefanya vyema kutoa maamuzi hayo.
Ole-Sendeka apingana na mamlaka ya usafirishaji wa Majini na Nchi kavu Sumatra
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment