Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamini William Mkapa amesema ipo haja ya kuitishwa mjadala wa kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa.
Mkapa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu hicho cha Dodoma Profesa Egid Mubofu na kumuaga Makamu Mkuu wa chuo hicho aliyemaliza muda wake Profesa Idrisa Kikula.
Mhe.Mkapa amesema mjadala huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta binafsi ama ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana.
Raisi Mkapa ipo haja ya kuitisha mkutano wa pamoja kujadili Elimu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment