Mbunge azuiwa kufanya mkutano kwasababu ya Mange Kimambi

Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chaha (CHADEMA) ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha polisi kutaka kuzuia mkutano wa Mbunge wa Tarime Vijijini CHADEMA, Mhe. John Heche kwa kile kinachodaiwa kuhofia maandamano yanayoratibiwa na Mange Kimambi.


Mara Ryoba amesema kuwa polisi wamekuwa na upendeleo kwa kuwa wanaona watu wa CCM wakiendelea kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa ili hali watu wa upinzani wakizuiliwa. 

"Haki huinua taifa; bali dhambi ni aibu ya watu wote. Nimepata taarifa kwamba Mbunge wa Tarime vijijini Mh. John Heche alizuiliwa asifanye mkutano Sirari eti kisa kuna maandamano ya Mange Kimambi, kwanza maandamano sio dhambi yapo kwa mujibu wa katiba yetu" alisema Mbunge Marwa Ryoba 

Kwa mujibu wa Mbunge wa Tarime Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA, John Heche amethibitisha hilo kuwa ni kweli kulikuwa na jaribio la kutaka kuzuiwa kufanya mkutano wake na wananchi wa Sirari kwa hofu ya maandamano ya tarehe 26 mwezi wa nne. 

"Ni kweli polisi walitaka kutuzuia kufanya mkutano ila pamoja na polisi Sirari kufanya jaribio la kutaka kuzuia mkutano wangu na wananchi, kwa kisingizio cha hofu ya maandamano ya tarehe 26. Mkutano wangu ulifanyika na umemalizika salama, Asanteni sana wananchi wa Sirari kwa kujitokeza kwenye mkutano wetu" alisema John Heche.
Mbunge azuiwa kufanya mkutano kwasababu ya Mange Kimambi Mbunge azuiwa kufanya mkutano kwasababu ya Mange Kimambi Reviewed by KUSAGANEWS on March 18, 2018 Rating: 5

No comments: