Rais wa Mauritius Ameenah Gurib-Fakim ametangaza kujiuzulu hapo jana huku kashfa ya kifedha ikiwa inaendelea kumuandama.
Gurib-Fakim ambaye alikuwa rais pekee mwanamke barani Afrika ameshutumiwa kwa kununua vitu binafsi vya kifahari vyenye thamani ya maelfu ya dola kwa kutumia kadi ya benki ya Taasisi ya Dunia yenye makao yake nchini Uingereza.
Gurib-Fakim alisema mapema wiki hii kwamba aliitumia kadi "bila kujua" lakini alikuwa amewarudishia fedha hizo.
Gurib-Fakim alichaguliwa kuwa rais mwaka 2015 na hapo awali alikuwa Profesa wa kemia katika kitivo cha sayansi cha Chuo Kikuu cha Mauritius.
Raisi wa Mauritius Ajiuzulu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment