Baada ya taharuki ya kisiasa ya karibu miezi minane, hatimaye Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa Nasa Raila Odinga wamekutana Ijumaa katika jumba la Harambe jijini Nairobi.
Kwenye kikao cha aina yake katika jumba la Harambee jijini Nairobi, wawili hao waliapa kushirikiana kuunganisha nchi ili kuondoa taharuki ya kisiasa ambayo imekuwepo tangu uchaguzi mkuu tata wa Agosti 8, 2017.
Kwenye hotuba fupi wawili hao walisema hakuna sababu yoyote kwa Wakenya kugawanyika kwa misingi ya kisiasa, kikabila ilhali hao ni ndugu.
Akimtaja Rais Kenyatta kama 'nduguye', Bw Odinga ameahidi kwamba kwa pamoja watasisitizia Wakenya umuhimu wa kuwa kitu kimoja.
"Tumekubaliana na ndugu yangu (Bw Kenyatta), Kenya iwe taifa moja ili kuzima migawanyiko iliyopo," amesema Raila ambaye Januari 30, 2018 alikula kiapo kuwa 'Rais wa Wananchi'.
Bw Raila alisisitiza uwepo wa kumaliza tofauti za kijadi ambazo zimekuwepo tangu Kenya ijinyakulie uhuru.
Kwa upande wake Rais, aliahidi kushirikiana kikamilifu na Bw Odinga.
"Tumegundua umuhimu wa viongozi kuja pamoja, kujadili maswala ya kitaifa yanayoikumba nchi. Tunawaomba Wakenya wote kujiunga nasi katika juhudi hizo," akasema Rais Kenyatta.
Kikao hicho kinaonekana kushinikizwa na wito wa Marekani, wawili hao kukutana ili kuzima taharuki ya kisiasa nchini.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni Alex Tillerson, anatarajiwa kuwasili nchini majira ya jioni leo Ijumaa katika juhudi za kuisaidia Kenya kufikia mwafaka wa kisiasa.
Rais Kenyatta akutana na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment