Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi likimalizana na Mwenyekiti wa Mtandao
wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo wamlete Dar es Salaam kwani amedai
haiwezekani akauchafua mkoa wake wa Dar es Salaam.
Paul Makonda amesema hayo leo na
kuwataka waandishi wa habari kutoandika habari ambazo hazijathibitishwa na
mamlaka husika kwani wanaweza kupelekea taarifa kwa umma ambazo zinaweza kuleta
taharuki kwa Umma.
"Juzi nimesikia sikia mmoja
anasema ametekwa mimi nafikiri wakimalizana naye kule Iringa watuletee hapa Dar
es Salaam, asituchafulie mkoa wetu na wengine wanaokimbia kuandika andika bila
hata kuwa na ushahidi kwamba mtu ametekwa, wewe watu wamefunga chuo wanarudi
majumbani kwao hata ikipotea network njiani fulani hatumuoni ametekwa ita
waandishi wa habari toa kauli ifike hatua niwaombe waandishi wa habari
angalieni taarifa mnazopeleka kwa Umma kama hazijathibitishwa na mamlaka husika
achaneni nazo tusitengeneze taarifa ambayo ikifika kwa Umma inaleta taharuki
isiyokuwa ya msingi" alisema
Paul Makonda
Abdul Nondo alitoweka katika
mazingira ya kutatanisha akiwa jijini Dar es Salaam na baadae kuripotiwa
kutekwa na watu wasiojulikana lakini alikuja kupatikana mkoani Iringa ambapo
imedaiwa alitupwa huko, jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya
tukio hilo la kutekwa kwa kijana huyo.
Mkimalizana Na Nondo huko Iringa Mtuletee huku Dar - Makonda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment