Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Arusha Bwana
John Palangyo amewataka wazazi kurudia majukumu yao ya awali ambayo tangu jumuiya hiyo inaundwa ilikuwepo
kwa lengo la kulinda maadili pamoja na kusimamia malezi, mazingira na Elimu
katika jamii.
Pallangyo amesema hayo katika hafla fupi ya kupokelewa
na jumuiya ya wazazi katika wilaya ya Arusha Mjini ambayo ilifanyika katika
ukumbi wa CCM mkoa wa Arusha ambapo jumuiya kutoka kata zote 25 za jiji la
Arusha zilishiriki.
Amesema kuwa kwasababu ya utandawazi uliopo kwasasa jamii
tayari imeshasahau elimu ya malezi hivyo wenye jukumu la kurudisha maadili hayo
katika jamii ni wazazi wote ambao hawapendezwi na mmomonyoko wa maadili katika
jamii.
Ameongeza kuwa elimu ya kidunia imeongeza maadili mabaya
ambayo hatujawahi kuwa nayo kama watanzania licha ya kuwa kipindi cha nyuma jumuiya
hiyo ilijisahau kiasi kwamba inajukumu la kusimamia maadili lakini sasa
wameanza kurudi kwenye mstari.
Naye Mjumbe wa baraza kuu taifa Arusha
Victor Mollel amesema maadili ya vijana yanapoharibika ni kwamba jumuiya ya
wazazi imeshindwa kuwajibika ni vyema wakaanza kushughilika mana kila mzazi ana
jukumu hilo.
Kwa upande wa Katibu wa wazazi wilaya ya Arusha Mjini
Christopher Pallangyo amesema katika kusimamia hilo suala la maadili wanatarajia
kufanya kongamano maalum tarehe 17 mwezi huu kwa lengo la kujadili suala la
mmomonyoko wa maadili kwa vijana na kuweka maazimio.
JUMUIYA YA WAZAZI CCM ARUSHA RUDIENI MAJUKUMU YENU YA MWANZO YA KURUDISHA MAADILI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment