Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander
Mnyeti ameliwezesha jeshi la polisi mkoani humo kwa kuwapa
matairi nane kwa lengo la kuendasha doria za kupambana na uhalifu
katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Mkuu huyo wa Mkoa amelitaka jeshi
hilo kutumia vifaa hivyo kwa haraka ili wasiipe hasara serikali ya kupoteza
askari watendaji pia kutoa taarifa pindi watakapoona hitilafu yoyote kwenye
vyombo hivyo vya moto na kuwahidi kuendelea kuongeza tairi zingine ili kazi ya
ulinzi izidi kuimarika.
Tairi hizo zinakadiriwa kuwa na
thamani ya shilingi milioni mbili laki moja na elfu sitini zimetolewa kwa lengo
la kuendesha doria za kupambana na uhalifu.
"Ambacho hatutaki ni,
mwenyekiti wa kitongoji alalamike, wa kijiji alalamike na ye mtendaji wa kata
alalamike halafu tuwasikie na nyie mnalalamika haipendezi, polisi wanapaswa
kufanya kazi. Serikali ni kubwa na ina wadau wengi wapo watatusaidia na
tutapata tairi nyingine. Tunawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya."
Mnyeti.
Mnyeti atoa Matairi nane kwa Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment