Rais Dkt. John Pombe
Magufuli amesema suala la maendeleo linapigwa vita sana hivyo amewataka
watanzania waunge mkono hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ili kuweza
kuimarisha uchumi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo
(Machi 09, 2018) wakati alipokuwa anafanya ufunguzi wa benki ya CRDB tawi la
Chato mkoani Geita.
"Niwaombe watanzania
tutangulize uzalendo kwanza, mahali popote tulipo tujue hatuna baba wala mama
hii ndio Tanzania yetu tukiichafua tumechafuka wote na maneno muda mwingine
huwa yanaumba. Nchi yetu inakwenda vizuri sana na mtu yeyote ukifanya vizuri
watu hawakupendi. Uzuri una gharama", amesema Dkt. Magufuli.
Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli
ameendelea kwa kusema "tunapoweza kujenga reli ya kisasa
(Standard Gauge) kwa Trioni 7.6 hela za ndani usifikili watu wanafurahi,
tunapoweza kuamua kujenga uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto rufiji
(Stieglers Gorge) tunapoweza kununua ndege 6 kitu ambacho tulikishindwa ndani
ya miaka 50 usifikili wengine wanafurahi".
ameendelea kusisitiza
"Maendeleo yanachangamoto na
vita kubwa ni lazima watanzania mjifunze na kuangalia mbele. Tumezungumza
Tanzania ya viwanda ila zipo nchi zilizolalamika eti ni kwanini sisi tuwe na
viwanda vya nguo kwa maana wanataka waendelee kutupa mitumba yao".
Kwa upande mwingine, Rais Dkt.John
Magufuli kesho (Machi 10, 2018) anatarajia kufanya ziara ya siku moja mkoani
Shinyanga, kukagua na kuzindua baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo barabara
inayounganisha Tanzania na Rwanda inayoanzia katika eneo la bandari kavu ya
Isaka wilayani Kahama hadi Rusahunga mkoani Kagera.
Rais JPM Maendeleo yanapigwa sana vita
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment