Polisi yatoa amri kukamatwa kwa Halima Mdee na Ester Matiko


Jeshi la Polisi Nchini leo Machi 22, 2018 limetoa amri ya kukamatwa kwa Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee pamoja na Mbunge wa jimbo la Tarime, Esther Matiko kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuitikia wito wa jeshi la polisi. 

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA imesema kuwa jeshi la polisi limeagiza wabunge hao wakamatwe popote walipo na kufikishwa kituoni kutokana na kushindwa kufika katika wito huo leo.

Aidha viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Mashinji na Salum Mwalim ambao walifika polisi kuitika wito huo mapema leo waliachiwa majira ya mchana wakiwa hawajahojiwa kitu chochote na kuambiwa warudi tena Jumanne 27, 2018.

Mbali na hilo jeshi la polisi liliendelea kuwashikilia Mbunge John Mnyika na John Heche ambao walibaki kituoni hapo na kufanyiwa mahojiano na kisha baadae kuruhusiwa kuondoka. 

Polisi yatoa amri kukamatwa kwa Halima Mdee na Ester Matiko Polisi yatoa amri kukamatwa kwa Halima Mdee na Ester Matiko Reviewed by KUSAGANEWS on March 22, 2018 Rating: 5

No comments: