Nondo apelekwa Iringa usiku, afikishwa mahakamani


Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesafirishwa usiku wa kuamkia leo Machi 21, 2018 kupelekwa mkoani Iringa.

Taarifa zilizotolewa na wakili wake, Jebra Kambole leo Jumatano Machi 21, 2018 zinaeleza kuwa sasa Nondo yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.

Nondo anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, 2018 na siku inayofuata akaonekana mjini Mafinga, wilayani Mufindi, Iringa ambako alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo na baadaye kurejeshwa Dar es Salaam.

Tangu akamatwe Nondo hajawahi kuzungumza na wakili wake wala mtu yeyote wa karibu yake jambo ambalo limekuwa likipingwa na watetezi wa haki za binadamu

Nondo apelekwa Iringa usiku, afikishwa mahakamani Nondo apelekwa Iringa usiku, afikishwa mahakamani Reviewed by KUSAGANEWS on March 21, 2018 Rating: 5

No comments: