Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa
(Basata), Godfrey Mngereza amesema mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond
amefanya makosa kumjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,
Juliana Shonza akifananisha kitendo hicho na kuitukana Serikali.
Diamond Platnumz na naibu waziri huyo waliingia katika vita ya maneno baada ya Serikali kufungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.
Akizungumza, Mngereza amesema Diamond anapaswa kuelewa kwamba maneno machafu anayoyatoa dhidi ya waziri huyo ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo hata ukienda katika sheria za kimtandao anaweza kujikuta anaingia matatizoni
Diamond, naibu waziri ni vuta nikuvute
Mngereza amesema wamesikitishwa na kauli ya
Diamond na kusisitiza kwamba ni vyema akafuata taratibu katika kulalamikia
suala hilo ikiwemo kuandika barua kama alivyomuelekeza Waziri Shonza
Ameongeza kuwa si lazima msanii aandikiwe
barua pale anapokosa kama ambavyo Diamond ameeleza katika ukurasa wake wa
Twitter, kwamba Shonza angemwandikia barua kabla ya kumfungia.
Amebainisha kuwa si kila mwanamuziki
anayefanya makosa huwa anaandikiwa barua
Katika malalamiko yake, Diamond amesema
naibu waziri huyo amekuwa akikurupuka kufungia nyimbo na pia kutowaandikia
barua rasmi ndio maana ameamua kuyazungumza kwenye redio na mitandao ya kijamii.
Jana Waziri Shonza alisema hawezi kujibizana
na Diamond kwa sababu alichofanya si maamuzi yake binafsi na kwamba kama anaona
ameonewa apeleke malalamiko yake kwa maandishi.
Basata Diamond amekosea kumjibu Waziri Shonza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment