Aliyeteka ndege ya Tanzania mwaka 1982 afariki dunia

Wakili nguli Yasin Memba anayedaiwa kuteka ndege ya Tanzania mwaka 1982 amefariki dunia jana Jumanne Machi 20, 2018 jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa wakili wa kujitegemea na mwanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) Mathew Kakamba, amesema Memba amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini humo.
Memba ni miongoni mwa watanzania wawili wanaodaiwa kuteka ndege ya Tanzania iliyokuwa na abiria 90, Februari 1982 wakishinikiza Rais wa wakati huo, Julius Nyerere kujiuzulu.
Aliyeteka ndege ya Tanzania mwaka 1982 afariki dunia Aliyeteka ndege ya Tanzania mwaka 1982 afariki dunia Reviewed by KUSAGANEWS on March 21, 2018 Rating: 5

No comments: