Wanafunzi wa darasa la saba ambao
watafanya mtihani mwaka huu watakutana na mabadiliko ya mfumo wa
utungaji wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi
Mabadiliko hayo yamefanywa na
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) jana na kutangazwa na Katibu
Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde.
Akizungumza Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi amesema mabadiliko hayo
aliyatangaza Dk Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na
wilaya unaofanyika Dodoma.
Nchimbi amesema katika muundo huo
mpya kila somo litakuwa na maswali 45, kati ya hayo, maswali 40 yatakuwa ya
kuchagua jibu sahihi na matano yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya
kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk
Amesema maswali 40 kila swali
litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili
huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali matano
yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.
Kutokana na muundo huo mpya, Necta
imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia mabadiliko
hayo ili kuwajengea uzoefu.
|
|
Necta wabadilisha Mfumo wa mtihani darasa la saba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment