WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka Mawaziri wa Afya kutoka
nchi tisa za Afrika kutoa mapendekezo ya namna ya kutokomeza magonjwa
yasiyoambukiza kwa wakuu wa nchi hizo ili yafanyiwe kazi.
Aliyasema hayo juzi wakati akifungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC)
Alisema magonjwa yasiyoambukiza ni miongoni mwa magonjwa ambayo yameendelea kuwatesa wananchi kwa kiasi kikubwa katika nchi nyingi za Bara la Afrika, hivyo vema mawaziri hao wakati mapendekezo ya namna ya kuyatokomeza.
|
Alisema magonjwa hayo yanaweza
kudhibitiwa kwa kuhamasisha wananchi kuboresha lishe na kusisitiza ulaji wa
vyakula bora, kufanya mazoezi na kubadili mitindo ya maisha.
|
“Magonjwa yasiyoambukiza
yanaongoza kwa kusababisha vifo katika baadhi ya nchi wanachama wa ECSA. Magonjwa
haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya mfumo wetu wa lishe na
maisha, hivyo ni muhimu suala hili likatafutiwa ufumbuzi.”
|
Waziri Mkuu alisema magonjwa
yasiyoambukiza pamoja na magonjwa mengine ya milipuko kama ebola, homa ya
bonde la ufa, dengue, homa ya manjano yamekuwa kikwazo cha maendeleo katika
baadhi ya nchi.
|
MAWAZIRI WA AFYA NCHI TISA KUTOA MAPENDEKEZO YA KUPAMBANA NA EBOLA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment