Waziri wa Mambo ya
ndani, Dk Mwigulu Nchemba amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa
wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na inapobidi matumizi ya fimbo
yatumike.
Akizungumza katika harambee ya
ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani
Singida, Dk Nchemba amesema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za
wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi.
"Kuna wakati walimu wananyoosha
nidhamu za wanafunzi lakini kuna watu wengine hawaoni haya ila wao ni
kulalamika tu, kinachofanyika ni kwa manufaa yetu. Niwaombe kwenye kutumia
mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo ili kutengeneza
taswira ya nchi yetu,"
amesema Dk Mwigulu.
Amesisitiza kuwa ni lazima kuendelea
kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya
madarasa.
Mbali na hayo Dk. Nchemba ameongeza
kwamba majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za
awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.
"Naunga mkono ujenzi huu
wa mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu
hivyo nachangia mifuko 200 ya saruji nawaahidi pia kutoa Sh milioni sita,"
alieleza.
Mwigulu ataka walimu kutumia viboko mashuleni kwa ajili ya maadili
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment