KAMANDA USALAMA BARABARANI MKOA WA ARUSHA AWASHAURI TANROAD

 Kamanda wa polisi usalama barabarani mkoani Arusha Joseph Bukombe ameiomba TANROAD wanapofanya ukaguzi wa maeneo ya ujenzi wa barabara kwa ajili ya kujenga miundombinu hiyo ni vizuri kupata ushauri kutoka  kwa askari kitengo cha usalama barabarani kwa ajili ya ushauri jinsi ya kuweka maeneo maalum ya vituo vya kushushia Abiria.

Akizungumza na wamiliki wa daladala AKIBOA pamoja na wasimamizi wa daladala DDA mkoa wa Arusha kamanda Bukombe amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa madereva wanaobeba abiria kukosa vituo vya Abiria.

“Ni kweli tumepata malalamiko hayo mfano barabara ya kuanzia Mbauda kwenda kwamurombo imenyooka tu hakuna kituo chochote cha kushusha abiria hili linafanya wakati mwingine madereva kuvunja sharia na kushusha abiria mahali popote “Amesema Bukombe

Bukombe amesema ameanza mazungumzo na mamlaka zinazohusika na miundombinu kutengeneza vituo vya kushusha abiria ili kuepuka kero baina ya askari na madereva.

Amesema kuwa wengi wanaojua matatizo ya barabarani ni askari pamoja na madereva ambao kwa muda wote wapo maeneo hayo na ndiyo watumiaji wa barabara hizo na kutokuwa na vituo vya kushusha abiria kumesababisha kuwa chanzo cha uvunjifu wa sharia.

Awali akizungumza mwenyekiti wa daladala Bille Matemu maarufu kwa jina la Kibosho amesema kuwa madereva wamekuwa wakitozwa faini na askari wanaposhusha abiria kwenye barabara hizo ambazo hazina vituo jambo ambalo limekuwa kero kubwa
KAMANDA USALAMA BARABARANI MKOA WA ARUSHA AWASHAURI TANROAD KAMANDA USALAMA BARABARANI MKOA WA ARUSHA AWASHAURI TANROAD Reviewed by KUSAGANEWS on March 24, 2018 Rating: 5

No comments: