Aliyekua Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amekosoa na kukemea mbinu zilizotumika kumuondoa madarakani na kudai kuwa amekua muhanga wa mapinduzi ya kijeshi.
Akiongea na televisheni ya Afrika Kusini Mugabe amesema kuwa Rais wa sasa Emerson Mnangagwa asingeweza kuingia madarakani bila kutumika kwa jeshi.
Rais huyo Mstaafu amesema alikua tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Emerson Mnangagwa na angehakikisha mabadiliko ya madaraka ya uhalali na si yale ya kulazimishwa.
Imeelezwa kuwa Mugabe amedai yupo tayari kwa ajili ya mazugumzo na Mnangagwa ili kulinda katiba yao na kwamba hakudhani kama angepoteza imani yake kwa Mnangagwa kwani yeye ndie alimsaidia kuingia serikalini.
''siamini kama yeye Mnangagwa angeweza kuniondoa madarakani , nimemuingiza serikalini, nimemsaidia alipokua jela anataka kunyongwa, sikuwaza kabisa kama siku moja yeye ndio atakua mtu wa kunitoa madarakani,'' Mugabe.
Mugabe aliondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo Novemba, 2017 akiwa na umri wa miaka 94
Mugabe akerwa na mbinu zilizotumika kumuondoa Kwenye Uraisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 16, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 16, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment