Wakazi wa Kivule wamelazimika kutumia kivuko cha miti kilichowekwa baada ya mvua kusomba daraja la muda, lililotengenezwa kupisha ujenzi wa daraja la Sirari katika mto Mzinga, Wilaya ya Ilala leo Machi 16 asubuhi.
Kivuko hicho hata hivyo kinaonekana kiko mbioni kusombwa na maji yanayozidi kuongezeka kufuatia mvua iliyonyesha jana jioni hadi usiku.
Daraja la Kivule lilisombwa na mvua Machi 8 mwaka huu na kusababisha adha kubwa kwa wananchi. Hii ni mara ya pili kwa daraja hilo kukatika ndani ya wiki moja kutokana na mvua zilizokuwa zimeambatana na upepo.
Kutokana na tatizo hilo vijana wamebuni mradi wa kuvusha watu kwa kuwatoza Sh 500 na pikipiki kwa Sh 2,000.
Mmoja wa Vijana hao ,Festo Songoro amesema kwamba ameanza kazi hiyo tangu alfajiri na hadi saa mbili alikuwa amevusha watu 20.

Wananchi wapata adha baada ya Kivuko cha Miti chasombwa na mafuriko
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 16, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 16, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment