Mbowe asema kifo cha Kimesera kimeleta pigo ndani ya Chadema

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimepata pigo baada ya kuondokewa na mmoja wa waasisi wake, Victor Kimesera.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe leo Jumapili Machi 25, 2018 imesema Kimesera alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH

Amesema Chadema kimempoteza mmoja wa watu wake muhimu waliokuwa nguzo ya ustawi wa chama hicho

 “Mzee Kimesera amekuwa katikati ya mapambano, tangu aliposhiriki kuasisi chama hiki, hadi mauti yalipomkuta akiwa mtendaji wa chama makao makuu. Tumepokea msiba huu kwa mshtuko mkubwa sana,” amesema

“Mzee Kimesera maarufu 'VPK' kama tulivyozoea kumuita, ametutoka kipindi ambacho mchango wake ungehitajika sana hasa wakati huu ambako taifa letu linapitia katika mkwamo mkubwa wa kisiasa,” amesema

Mbowe amesema Kimesera atakumbukwa zaidi kwa namna alivyojitolea kwa hali na mali kupigania haki, demokrasia na maendeleo nchini hususan katika Jimbo la Kiteto mkoani Manyara

Amesema kwa sasa Chadema kupitia ofisi ya katibu mkuu, inashirikiana na familia ya marehemu kupanga taratibu za mazishi

 “Taarifa nyingine ikiwAmo ratiba ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, zitaendelea kutolewa,” amesema
Mbowe asema kifo cha Kimesera kimeleta pigo ndani ya Chadema Mbowe asema kifo cha Kimesera kimeleta pigo ndani ya Chadema Reviewed by KUSAGANEWS on March 25, 2018 Rating: 5

No comments: