Mwenyekiti wa Taifa wa
Chama Cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amefunguka na
kuweka wazi kuwa Jumapili hii ya matawi imekuwa ni njema kwake na imemuongezea
nguvu na ujasiri mpya kuendelea kutetea haki nchini Tanzania.
Mbowe amesema hayo mara baada ya
kutoka katika misa ya Jumapili ya matawi ambapo yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati
Kuu ya (CHADEMA) Mhe. Edward Lowassa waliweza kusali katika kanisa la Kilutheri
Azania Front jijini Dar es Salaam.
"Neno lililotawala leo Jumapili
ikiwa ni Jumapili ya Matawi (Mtende) siku 7 kabla ya kufufuka Mesiah, Bwana
Yesu Kristo ambayo ni Sikuu Kuu ya Pasaka, lilikuwa ni amani, ili amani
ipatikane lazima haki katika familia, haki ndani ya jamii ipatikane, haki uinua
taifa, bila haki hakuna amani, hakuna upendo, watawala wajue wakiiminya haki
basi wajue hakuna amani,amani ni muhimu sana" alisema Mbowe
Aidha Mbowe aliendelea kusema kuwa
"imekuwa Jumapili njema kwangu na iliyonijaza nguvu na ujasiri mpya wa
kuendelea kuitetea haki, nawatakia Jumapili njema ya Matawi.
Freeman Mbowe jumapili ya Matawi yamfanya kuanza upya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment