MBARAWA AWATAKA WANAOISHI MABONDENI KUHAMA MARA MOJA

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewataka watu wanaoishi mabondeni waliogoma kuondoka baada ya kupata taarifa juu ya hatari inayowanyemelea kuondoka mara moja ili kuepusha majanga

Akizungumza leo Machi 23, Mbarawa amesema hivi sasa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) inatoa taarifa za hali ya hewa inayowataka walioko katika maeneo ya mabondeni lakini hawako tayari kuondoka 

“Unapopata taarifa ya hali ya hewa kama mahali hapo si lazima maana yake ni lazima uondoke, vinginevyo utapata shida,”amesema Amesema lazima kufuata utabiri wa hali ya hewa ili kujiepusha na majanga yanayoweza kujitokeza kwa kudharau taarifa zinazotolewa na mamlaka hiyo Amesema zingatia taarifa hali ya hewa ndio kaulimbiu ya maadhimisho yaliyofanyika jana yakilenga watu kutopuuza utabiri wa hali ya hewa

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema makubaliano ya kimataifa ni kuwa na utabiri wenye usahihi kwa asilimia isiyopungua asilimia 70

“Utabiri wetu sasa umeongezeka usahihi tumefika hadi asilimia 88 wakati mwingine tunafika asilimia 90,”amesema

Aidha, amesema wamekuwa wakishirikiana na taasisi nyingine nchini katika kuchukua hatua wanapotoa taarifa za kutahadharisha watu.
MBARAWA AWATAKA WANAOISHI MABONDENI KUHAMA MARA MOJA MBARAWA AWATAKA WANAOISHI MABONDENI KUHAMA MARA MOJA Reviewed by KUSAGANEWS on March 23, 2018 Rating: 5

No comments: