Aliyekuwa Spika wa Bunge
Bi. Anna Makinda ameshauri madiwani wanawake kuhakikisha wanajenga hoja
zitakazozifanya halmashauri zao kuwatambua wanawake walio nje ya mifumo ya
kifedha ili kuwasaidia kupata mikopo inayotolewa kupitia fungu la uwezeshaji.
Mama Makinda ameto wito huo jijini
Dar es Salaam leo na kufafanua kuwa asilimia kumi ya fedha zinazotengwa na kila
halmashauri nchini zimelenga kuwainua kiuchumi wanawake hao ambapo hawapo
kwenye vikundi kama VICOBA, SACCOS na aina nyingine za makundi ya
kijasiriamali.
Akifafanua hoja hiyo, Spika huyo
mstaafu ameshauri njia nyingine ambayo madiwani wanawake wanaweza kuitumia kuwa
ni kupitia mabaraza ya madiwani ambako wanatakiwa kutoa ushauri wa kuongeza
vyanzo vya mapato.
Amesema ili hiyo asilimia kumi
inayotengwa kuinua wananchi kiuchumi iwe ya kutosha na kuwafikia wahitaji wengi
zaidi wanahitajika kupaza sauti zao.
Mama Makinda ashauri madiwani wanawake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment