Majaliwa awataka wafanyabiashara kukopa


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara wilayani hapa kutumia taasisi za fedha kukopa kwa ajili ya kukuza mitaji yao
Ameyasema hayo leo Jumapili Machi 25, 2018  wakati akizungumza na wafanyabiashara wa wilaya hiyo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Chama Cha Walimu (CWT) Ruangwa

Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, amesema ni vyema wakatumia taasisi za fedha zilizopo ili kukuza mitaji yao

”Naamini sekta ya biashara ni muhimu katika mabadiliko ya maendeleo, hivyo wafanyabiashara ni chachu ya maendeleo kokote na Serikali itaendelea kuwaunga mkono.” Amesema

Amesema katika kuhakikisha riba zinapungua, Rais  John Magufuli anaendelea kuzungumza na wamiliki wa taasisi za fedha ili waone namna ya kupunguza riba hizo

Naye  mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara Wilaya ya Ruangwa,  Said Shea amewaomba wenzake kutumia fursa za maendeleo zilizopo wilayani humo kwa kupanua wigo wa biashara zao.

Majaliwa awataka wafanyabiashara kukopa Majaliwa awataka wafanyabiashara kukopa Reviewed by KUSAGANEWS on March 25, 2018 Rating: 5

No comments: