Kampeni ya kupima Ukimwi wanaume yaja


Baada ya utafiti kubaini mwamko mdogo kwa wanaume kupima nakutumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARVs), Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) sasa kuanzisha kampeni maalumu

kizungumza leo Jumapili Machi 25, 2018 na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Kupambana na Dawa za Kulevya, mkurugenzi mkuu Tacaids, Dk Leonard Maboko amesema kampeni hiyo itakuwa miongoni mwa shughuli zitakazofanywa katika mkakati wa nne wa kupambana na Ukimwi nchini

“Katika utafiti wa mwaka 2016/17, tuliangalia vitu vipya ambavyo ni maambukizi mapya na kiwango cha kufubaza VVU.

Tuligundua ingawa wanawake wanaongoza katika maambukizi mapya, lakini ni wepesi kupima na kutumia dawa kikamilifu ndiyo maana kwenye kiwango cha kufubaza wanaongoza,”amesema

Amesema katika utafiti huo uliozinduliwa Desemba mwaka jana, kiwango cha watu kufubaza VVU kwa wenye miaka kati ya 15 na 64 ni asilimia 52 lakini kati ya hao, 57.5 ni wanawake na wanaume ni 41.2

Amesema kwa mujibu wa Mkakati wa Taifa wa Ukimwi unaoishia mwaka huu gharama za kugharamia Ukimwi nchini zinakadiriwa kufikia Sh6 trilioni kwa muda wa miaka mitano

Naye waziri wa nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Jenista Mhagama amesema mwaka 2015 wafadhili wa tume hiyo walianza kupunguza fedha za mapambano dhidi ya VVU.

Kampeni ya kupima Ukimwi wanaume yaja Kampeni ya kupima Ukimwi wanaume yaja      Reviewed by KUSAGANEWS on March 25, 2018 Rating: 5

No comments: