Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu
imekubali hoja 3 kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu katika kesi ya Babu Seya
ikiwemo hoja ya Nguza Viking kutaka apimwe nguvu za kiume.
Akisoma hukumu kwa niaba ya majaji wenzake,
Jaji Gerard Niyungeko aliainisha kwamba kati ya haki zilizokiukwa wakati wa
mwenendo wa kesi hiyo ni ombi la Nguza Viking kupimwa kitabibu ili kuthibitisha
kama hakuwa na nguvu za kiume na hivyo asingeweza kufanya vitendo vya ubakaji.
Mahakama hiyo imekubali pia hoja kwamba
Viking (maarufu kama Babu Seya) na mwanaye, Johnson Nguza (maarufu kama Papii
Kocha) hawakupata maelezo ya mashahidi wala fursa ya kuwahoji walotoa ushahidi
ili kuthibitisha makosa.
Hata hivyo, hoja nyingine mbalimbali
ziliwekwa kando ikiwemo hoja ya watuhumiwa hao kutolewa gerezani, huku mahakama
ikisema kwamba tayari wameshatolewa kwa msamaha wa Rais John Magufuli.
Je, mahakama imesemaje kuhusu fidia, ama
kuhusu uendeshaji wa kesi hiyo? Fuatilia zaidi stori hii katika Kusaga News kesho
na kupitia Blog yetu ya kusaganews.
Mahakama yakubali hoja 3 kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu katika kesi ya Babu Seya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment