Jeshi la polisi Mkoani
Dodoma linawashikilia watuhumiwa 14 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu wakiwemo
matapeli waliojifanya kuwa ni maofisa ununuzi kutoka Jeshi la Wananchi wa
Watanzania (JWTZ) na maofisa usalama wa Taifa.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa
Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake na kusema watuhumiwa hao walikamtwa kwenye mitaa mbalimbali ya
Mkoa wa Dodoma wakifanya vitendo vya uhalifu baada ya kumtapeli mfanyabishara
mmoja kiasi cha sh. Million 8.
Waliokamatwa katika tukio hilo ni Shaaban
Kwiyela (58) Mkazi wa Kijiji cha Igunga Mkoani Tabora, ambaye alifukuzwa kazi
kwa utovu wa nidhamu tangu mwaka 1995 akiwa kikosi cha 36KJ Msangani
Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha sajenti lakini amekamatwa akiwa na mavazi
ya cheo cha Kaptein.
Wengine ni Emmanuel Michael (45)
mkazi wa Iringa, Juma Pesambili (33) Mkazi wa Sai Mbeya na Emmanuel Mwagonela
(50) Mkazi wa Mtaa wa Ghana mkoani Mbeya.
POLISI WASHIKILIA WANNE KWA KUJIFANYA MAOFISA UNUNUZI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment