Jeshi la Polisi linaendelea na msako dhidi
ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara na mmiliki wa
kampuni ya mabasi ya Super Sami, Josia Mzuri maarufu kwa jina la Samson ambaye
mwili wake ulikutwa kwenye viroba ndani ya Mto Ndabaka mpakani mwa wilaya za
Bunda na Busega
Akizungumza kwa njia ya simu leo Machi 23,
Kamanda wa Polisi mkao wa Mara, Jaffari Mohamed alisema pamoja na msako dhidi
ya watuhumiwa wengine, jeshi hilo pia linaendelea kuwahoji watu wanne
wanaoshikiliwa kuhusiana na tukio hilo
Ametoa wito kwa wenye taarifa zitakazosaidia
kuwanasa wahusika au kufanikisha ushahidi dhidi ya watuhumiwa wanaoshikiliwa
kujitokeza kuziwasilisha polisi
“Suala hili linahitaji uchunguzi wa kina si
tu kubaini na kuwanasa wahusika, bali pia kupata ushahidi wa kina unaotosheleza
kuwatia hatiani, tunaomba raia wema washirikiane na polisi kukamilisha jukumu
hilo,” amesema Kamanda Mohamed.
“Mauaji haya yameibua hofu na wasiwasi mwingi miongoni mwetu wafanyabiashara ya usafirishaji wa abiria mkoani Mwanza kwa sababu hatujui kwanini mwenzetu katekwa na kuuawa wala hatuelewi nani atafuata,” alisema Msukuma
Mfanyabiashara huyo alitoweka tangu Februari 27, siku moja baada ya kushiriki kikao cha Kamati ndogo ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), mkoani Mwanza kilichofanyika jijini Mwanza Februari 26
Gari la mmiliki huyo wa mabasi, Machi 9 lilikutwa likiwa limeteketezwa kwa moto ndani ya eneo la eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara, siku tano kabla ya mwili wake kukutwa ndani ya maji katika Mto Ndabaka ukiwa umefungwa kwenye viroba.
MSAKO WAENDELEA KWA WALIOMUUWA MMILIKI WA MABASI SUPER SAMI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment