Mahakama Kuu Kanda ya
Dar es Salaam imemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuleta majibu kuhusu
mashauri mawili ya kikatiba yaliyofunguliwa mahakamani hapo na wanaharakati
dhidi ya ofisi yake, ifikapo Machi 21 mwaka huu.
Mashauri hayo ni,
shauri namba 4/2018 linalopinga sheria ya jeshi la polisi na ya vyama vya siasa
zinazodaiwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, na shauri namba 6/2018
linalopinga sheria ya uchaguzi inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri
nchini (maded) kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Hayo yamebainishwa leo
mahakamani hapo na Mwanasheria upande wa walalamikaji, Wakili Jebra Kambole
baada ya kuairishwa kutajwa kwa tarehe za kesi hizo kufuatia majaji
wanaosikiliza kutokuwepo mahakani kwa sababu ya kuwa na dharula.
Vile vile, Wakili
Kambole amesema mahakama imetaja tarehe 5 Aprili, 2018 kuwa siku ya kutajwa
tarehe za kesi hizo.
“Mahakama imetoa amri
mbili, kwanza imetaja terehe 5 mwezi wa 4 haya mashauri yatakuja kutajwa
tarehe, imetoa amri ya pili kwa mwanasheria mkuu wa serikali kwamba anapaswa
kuleta majibu yake tarehe 21 mwezi wa 3, 2018 kwa hiyo hizo ni amri mbili
zilizotolewa na mahakama siku ya leo. “
Amesema miongoni mwa
walalamikaji katika shauri namba 4/2018 ni Baraka Mwago, wakati shauri namba
6/2018 mlalamikaji ni Bob Chacha Wangwe.
“Tulichokuja leo ni
kuangalia namna gani mahakama itatoa amri ili watu mbalimbali waweze kutimiza
wajibu wao, ni mashauri ya kikatiba yanapinga sheria mbalimbali ikiwemo sheria
ya uchaguzi ambayo inafanya maded kuwa wasimamizi wa uchaguzi wakati inapaswa
kuwa na tume huru ya uchaguzi, shauri namba nne inapinga sheria ya jeshi la
polisi na sheria ya vyama vya siasa ambazo zinazuia mikutano ya vyama vya siasa
na kuleta madharakwa wanachi. Tunapinga sheria hizo tunaona ni kandamizi
zinakiuka katiba ikiwemo ibara ya 18 inayoruhusu uhuru wa kujieleza,” amesema
na kuongeza.
Na Regina Mkonde
MAHAKAMA KUU YAMUAGIZA MWANASHERIA MKUU KUHUSU MAANDAMANO TANZANIA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment