|
Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo amesema mabaraza ya
vyama vya siasa yakitumika kikamilifu yanaweza kuondoa malalamiko ya wananchi
na viongozi wa upinzani.
Amesema hayo leo Machi 11,2018 akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu vuguvugu la maandamano
yaliyopangwa kufanyika Aprili 26,2018 yanayoratibiwa kupitia mitandao ya
kijamii.
Cheyo amesema maandamano hayo ni uchochezi na uvunjifu
wa amani na kwamba, mambo yanayolalamikiwa yangeweza kutatuliwa kupitia
mabaraza hayo
"Tusitake kufika hatua ya kuandamana barabarani
ili kudai haki, Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi. Tukifikia huko amani
iliyopo Tanzania tutashindwa kuipata tena na wananchi watakosa nchi nyingine
yenye amani ya kukimbilia," amesema.
Cheyo amesema kama tatizo ni fedha kwa ajili ya
mabaraza hayo kukutana, Rais John Magufuli anapaswa kutoa fedha kuyawezesha
kufanya vikao
"Siungi mkono hoja za kudai kuwepo mikutano ya
hadhara hata kama ni kwa ajili ya kuongeza wanachama kama wanavyodai wengine,
naamini kwa sasa mitando ya kijamii ina nguvu kuliko kitu chochote
nchini," amesema Cheyo.
Amesema kabla ya kudai haki ya kuandamana, zipo
nyingine wananchi wapaswa kuzipa kipaumbele zikiwemo haki ya kuishi, kupata
maji safi na salama, elimu na afya
"Hatuwezi kufika mahali tuseme nchi hii imepotea
na hakuna demokrasia kisa tumekosa haki ya kuandamana, haki ya kufanya
mikutano ya hadhara. Kila mtu alishuhudia mikutano ya kampeni za uchaguzi wa
ubunge wa marudio katika majimbo ya Kinondoni
na Siha ilivyogeuka sehemu ya
kutukanana," amesema Cheyo
"Kama kitu mnachokidai kiliweza kusababisha watu
kugombana na askari hadi mauaji yakatokea hicho kitu hakitusaidii kama
nchi," amesema.
Cheyo amesema yanayodaiwa kwa nguvu hayana faida na
manufaa ya kila siku kwa sababu watu wanahitaji kupata wakati wa kulima na
kuvuna
"Hiyo mikutano iliyoshupaliwa sasa na kuhitajika
kwa nguvu zote si kweli kwamba kila siku watakuwa barabarani kuhutubia
wananchi, fedha tutatafuta saa ngapi, tutalima saa ngapi, hivyo ni vyema
tutambue kila kitu kinachofanyika kupitia mambo ya siasa kisiwe kisingizio
cha kusema nchi haina amani, haina uhuru," amesema Cheyo.
Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwa kiunganishi
cha wananchi na viongozi wa vyama vya siasa na si kufanya kinyume cha hilo.
|
||
|
|||
Maandamano yanayotakiwa kufanyika ni Uchochezi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment