Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea
amesema amepeleka bungeni barua ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kuwa
na chombo huru cha kusimamia uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo Jumapili Machi 11,2018 Kubenea amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) si
chombo huru cha kusimamia uchaguzi.
Amesema barua hiyo aliiwasilisha
Alhamisi Machi 8,2018 katika ofisi ya Katibu wa Bunge mjini Dodoma.
Kubenea amesema uchaguzi kusimamiwa
na Tume isiyo huru inaweza kusababisha machafuko
"Hatuwezi kuacha hali hii
iendelee, vurugu zimekuwa zikitokea kwa sababu ya kuwa na Tume ya aina hii,
tunataka chombo huru," amesema
Kubenea awasilisha hoja Binafsi Bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment