Rais John Magufuli amemwagiza
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
kuhakikisha wamiliki wa viwanda vya ndani wanaajiri wazawa.
Ametoa agizo hilo akizindua
kiwanda cha kufua vyuma cha Kahama Oil Mill mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Rais amesema wananchi wazawa ndio
waliompigia kura, hivyo wapewe kipaumbele cha ajira katika viwanda hivyo
“Kama wewe ni waziri nimekuteua
mimi, unaacha kuwaajiri wazawa walionipigia kura unaenda kuchukua watu
wa nje hii hakubaliki,” amesema.
Rais Magufuli amesema, “Nitoe wito
kwa mawaziri wangu na wakurugenzi, hakikisheni viwanda mnavyovianzisha nchini
mnaajiri Watanzania, hawa ndio walionipigia kura.”
Amewataka wamiliki wa viwanda
kuhakikisha wanatumia malighafi za ndani kutengeneza bidhaa badala ya kuagiza
kutoka nje ya nchi
“Mwaka huu pamba nyingi imelimwa,
Kahama Oil Mill pia mnatengeneza mafuta, hakuna haja ya kuagiza pamba kutoka
nje wakati tuna pamba ya kutosha hapa,” amesema
Kuhusu kiwanda cha chuma
amesema malighafi inapatikana nchini, hivyo iwapo mkurugenzi wa
Kahama Oil Mill anahitaji yupo tayari kumpa bure badala ya kuagiza nje
Pia, amewataka Watanzania kununua
bidhaa za ndani, huku akiwataka wamiliki wa viwanda kutengeneza zenye ubora
ili kuhimili ushindani.
|
|
Magufuli atoa Agizo kuhusu ajira kwa wazawa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment