MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA KATA WALALAMIKIWA MERU MBELE YA MWENYEKITI WA UWT ARUSHA.

Jumuiya ya wanawake jimbo la meru mkoani Arusha wamewalalamikia maafisa maendeleo wa kata kwa kutotimiza wajibu wao katika na wengine
kutoonekana kabisa wakidai kuwa wanafanya shughuli zao binafsi na kusahau wajibu wao wa kuwatumikia wananchi.

Wanawake hao zaidi ya 200 wakizungumza mbele ya mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake mkoani Arusha Bi Yasmini Bachu wamelalamika kuwa maafisa
hao wamekuwa kero kwasababu hata elimu ya Ujasiriamali na utaratibu wa kujiunga kwenye vikundi ili wapate mikopo ya serikali hawaipati .

Wamesema kuwa wanapohitaji elimu ya ujasiriamali baadhi ya maafisa hao huwataka walipe fedha kinyume na utaratibu kwani wao ni waajiriwa wa serikali walipaswa kutoa huduma hiyo kwa wananchi bure.

Vile vile wameongeza kuwa kumekuwa na gharama kubwa na usumbufu wakati wa kusajili vikundi jambo linalowakatisha tamaa kwani hawawezi kupata
mikopo ya serikali bila kusajili vikundi vyao
Kwasasa halmashauri ya Meru haina utaratibu wao wenyewe wa kusajili vikundi kama ilivyo kwa halmashauri ya ARUSHA DC badala yake vikundi
vyote vinasajiliwa na Brella Dar es salaam jambo linalopelekea vikundi vya akina mama kutumia Laki moja na 20 hadi laki moja na nusu kama
gharama ya kusajili vikundi

Akitoa mafunzo nakujibu maswali ya akina mama hao wa Meru afisa maendeleo way jamii Ndugu Mrema amekiri kupokea malalamiko hayo kutoka
kwa akina mama na kuahidi kuyafanyia kazi.

Akijibu suala la Gharama za kusajili vikundi Afisa maendeleo huyo amekiri vikundi vyote kusajiliwa Brella kwasasa wakisubiri baraza la madiwani la Meru kupitisha utaratibu wa halmashauri kusajili vikundi yenyewe kwa gharama nafuu.

Hata hivyo amewaomba akina mama hao wasitoe tena fedha bali watoe taarifa za wale maafisa wanaofanya tabia hiyoya kutoza fedha ili wachukuliwe hatua kwa kuwa ni jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu.

Kwa halmashauri ya Meru hadi kufikia sasa imetoa mikopo kwa vikundi vya vijana na akina mama 74 zaidi ya milioni 162.5.

Akizungumzia suala hilo mwenyekiti wa Uwt Yasmini Bachu ataendelea kuishaur halmashauri kuhakikisha inatenga asilimia kumi ya mapatoyake ya ndani kila mwezi na kuyaelekeza kama mikopo nafuu kwenye vikundi ya vijana na akinamama kama ilivyoelekezwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi 2015/2020.

Ziara ya mwenyekiti Bachu kukutana na viongozi wote wa kata na matawi itaendelea halmashauri ya jiji la Arusha Tarehe 28/03/2018 saa nne asubuhi ukumbi wa CCM mkoa.

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA KATA WALALAMIKIWA MERU MBELE YA MWENYEKITI WA UWT ARUSHA. MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA KATA WALALAMIKIWA MERU MBELE YA MWENYEKITI WA UWT ARUSHA. Reviewed by KUSAGANEWS on March 20, 2018 Rating: 5

No comments: