Vyama vya michezo kujisalimisha

Baraza la Michezo nchini (BMT) limevitaka vyama vya michezo ambavyo mpaka sasa havijawasilisha kalenda yao ya matukio ya mwaka kujisalimisha kwaajili ya kutoa maelezo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.

Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari amesema, licha ya kuongeza muda mpaka Februari 28 mwaka huu lakini mpaka sasa ni vyama 17 pekee kati ya vyama zaidi ya 50 vilivyopo hapa nchini ndivyo vilivyowasilisha Kalenda zao za mwaka huu.

“Hali inasikitisha na vyama vinalazimisha sheria ifuate mkondo wake, mpaka sasa hivi pamoja na kuongeza muda lakini vyama vimekuwa ni vigumu sana kuleta kalenda, kwahiyo wito wangu kwa leo chama ambacho kinajua hakijaleta kalenda kijisalimishe chenyewe'', amesema Bakari.
Aidha Bakari ameongeza kuwa kwa sasa wanaandaa barua za wito kwa vyama hivyo kabla ya hatua kuchukuliwa na kuna barua ambazo tutatoa kwaajili ya maelekezo kwamba ni nini wanatakiwa kufanya.


Bakari amemaliza kwa kusema utaratibu wa sasa kwa vyama ambavyo vitawahi kufika BMT vitatakiwa kutoa maelezo kwanini wamekaidi agizo la Baraza huku akiongeza kuwa Barua zitawafikia wote ambao hawajawasilisha kalenda zao.
Vyama vya michezo kujisalimisha Vyama vya michezo kujisalimisha Reviewed by KUSAGANEWS on March 20, 2018 Rating: 5

No comments: